

W A T E N G W A
有意識的音樂. musique consciente . ደኅና ሙዚቃ. Muziki fahamivu. واع موسيقى .




"Lakini ukiwa mbele, mtizame wa nyuma yako, unaweza ukajikwaa akakuacha nashida zako" - Donii
አምደኛ Taarifa rasmi 官方消息
New Album release 2017
Safari ya HipHop
Safari ya HipHop album is the journey of JCB, Yuzzo and Dwee from Watengwa back to France. Along the way they met and featured other artists such as Tina Mweni and Robah Wenyeji from Kenya, Frost from Tanzania, as well as Boss One, K-Méléon and Les Crevards from Marseille, France.
JCB na Mo+ kutoa Makalla wa Ukoo album mixtape
Jcb ametoa taarifa kwamba, yuko katika mchakato mkali wa kutoa album mixtape itakayokwenda kwa jina la Makalla wa Ukoo. Jcb amesisitiza kuwa mix tape hio ambayo wanaifanya yeye na Mo plus ndani ya studio za noize maker,wameshakamilisha kutengeneza ngoma kama kumi hivi na lengo lao halisi ni kwamba, zifike ngoma kumi na tano. Jcb amesema katika kukamilisha kazi hiyo wametumia, beat za maproduza tofauti tofauti kama vile Dx, Kz ambaye yuko sweden(ziggy lah), Chindo, Mosco, John bee, na Dj Azii ambaye yuko India. "Ndani ya hiyo album utampata chindo, donii,chaba frost....so wana wa kitaa wakae mkao kupata madini toka kwa Mo plus na Jcb..ambayo hii album tunaidedicate kwa mchizi wetu Lexa ambaye tulikuwa naye bega kwa bega kabla hajafariki" Alisema Jcb. (Kushoto ni picha ya Jcb, Saigon na Mo Plus a.k.a Baba wa ukoo)
Watengwa live radio interview in france
WATENGWA est un collectif hip hop d’Arusha en Tanzanie, un groupe dont les principaux MCs, dont plusieurs des membres fondateurs du crew en 2000, sont en France en ce moment dans le cadre du programme EARU (East Africa Rise Up) initié par une association française.
Concerts (à L’Équitable Café vendredi 18 mai) et enregistrement d’un nouvel album entre Paris et Marseille, diffusion de titres exclusifs et palabres hip hop. Listen live interview here
Tuchangie ‘Ni Full Ile Laana Vol. 2′ kutoka Utengwani
Na Tzhiphop.com,
Watengwa wamepata nafasi ya pekee kwenda Paris, Ufarasa, mwishoni mwa mwezi huu (Aprili). Ukiacha nafasi ya kutumbuiza sehemu kadhaa, watatumia safari hii kurekodi “Ni Full Ile Laana Vol. 2″, kutengeneza video za nyimbo kadhaa na filamu itakayotanabahisha shughuli zao. Huu ni mradi wa East Africa Rise Up, kati ya Ufaransa na Afrika Mashariki. Mradi mzima utachukua takribani mwezi mzima.
Zimebaki takribani siku sita watu, mashabiki na wapenzi wa Hip Hop Tanzania kuchangia kile walichonacho ili kufanya ndoto za Watengwa kuwa kweli! Bofya hapa ili uchangie na kuona kile utakachopata kulingana na kiasi utakachotoa.
Ili kupata undani wa zoezi zima, tuliwasaka JCB na Chindo, na mahojiano yalikuwa hama ifuatavyo…
1. Vipi mzee, mara ya mwisho ulitutaarifu kuhusu kampeni yenu ya kuwaasa wana wa Arusha kuachana na vurugu za silaha hasa visu, mnaendeleaje?
[JCB] Kampeni za Arusha Bila Visu zilianza mwaka jana mwezi wa tatu, baada ya kutokea kifo cha Izz Pacha… na ndio mwezi aliofariki Faza Nelly pia. Tukaona mwezi wa tatu kila mwaka tutakuwa tunatumia muda huo kuwakumbuka ndugu zetu waliotutoka kwa njia ya kuchomwa kisu. Wako wengi kuliko hao tuliowataja…
Kwa hiyo hizi kampeni ni za kila mwaka. Mwaka huu tumetengeneza wimbo, wasanii nane wa pande za Arusha na Nairobi… wimbo unaitwa “Arusha Bila Visu Inawezekana”. Mwaka huu tulipanga pia kufanya tamasha lakini tulikosa wadhamini, ila hatujakata tamaa sababu kila mwezi wa tatu itakuwa ni mwezi wa Arusha Bila Visu Inawezekana. Tusububiri mwakani tuone.
2. Wewe uko mbali lakini kiroho unaonekana bado upo Arusha, kuna changamoto zozote unazozipata wakati unajaribu kufuatilia kinachotokea ulipotoka?
[Chindo] Kwanza, nashukuru sana kwa nafasi hii. Kuhusu changamoto nazozipata nikifuatilia nilikotoka, ziko nyingi sana. Kama ulivyosema kiroho niko Arusha, kimwili niko narekebisha maisha. Changamoto kubwa ni kuona mapengo mengi sana katika game la Arusha. Kwanza kabisa, umoja wa ma-emcee umepotea, na kujisahau. Nafurahi sana kuona kamanda wangu, General, Degree JCB akiwa katika level ya juu na kuendeleza misingi. Nasikitika na kuchukia wasiompa support kwa kuwa yeye ndio Godfather wa Hiphop Arusha… na marehemu Faza, Rest In Freedom. Makapteni wa Arusha tunahitaji kuunda “Arusha Hip Hop Community”, ambayo itasaidia kutatua matatizo yetu kuhusiana na kazi zetu. Pia tusisahau tulipotoka siku zote. Zaidi hapa
Documentary "Watengwa 2 France, a Musical Safari"
Original documentary about the trip of JCB, Chondo, Yuzzo and Frost (TGP) to France (Paris, Cergy, Marseille)..










